Tofauti na jinsi mheshimiwa alivyokabidhiwa nchi na mtangulizi wake, Hali inaashiria kuwa tofauti sana kwa jinsi yeye atakavyomkabidhi mrithi wake.

Ni wazi mrithi wa Kikwete atakuwa na kazi ngumu sana kuukarabati mfumo tawala wa taifa hili uliojengwa kwa NEPOTISM, CRONISM na UDINI wa awamu hii ya nne ya uongozi wetu.

Aidha kwa jinsi wengi walioko au wanaodhamiwa na mfumo huu wa awamu ya nne walivyojitajirisha kwa CORRUPT and ILLEGAL DEALS, Ni wazi pia kuwa mrithi ajaye wa JK atapata taabu sana kufanya mambo wasiyoyakubali (Yanayotishia maslahi yao).

Lakini pia Kwenye siasa za kimataifa kuna hofu kuwa huenda safari nyingi zaidi ya mia nne za kiongozi huyu hazikuwa kwa maslahi mapana ya taifa, na hivyo kama mrithi huyo atakwenda kinyume chake pia akasusiwa kwa namna fulani.