HALI bado ni tete kwa mwenyekiti wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini wakakosa ajira, George Mgoba kufuatia kutekwa kwake na kujeruhiwa vibaya hivi karibuni na watu ambao bado hawajajulikana.

Mwenyekiti wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini wakakosa ajira, George Mgoba akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Mgoba ambaye mpaka juzi alikuwa bado amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana jiijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa, simulizi yake inaonesha kichwani kumejaa msongo mkubwa wa mawazo kutokana na watu waliomteka kumlazimisha kufanya mapenzi na mwanamke mmoja.